Katibu wa CCM apata kipigo kutoka kwa wanachama wake

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi kata ya Bugogwa wilayani Ilemela, leo asubuhi wamevamia katika ofisi za wilaya hiyo na kumshabulia kwa kipigo katibu wa chama hicho wilayani humo Bw. Acheni Maulid wakipinga kukatwa kwa jina la mgombea aliyeshinda kwenye kura za maoni kwa madai kuwa ni mkimbizi.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 5 asubuhi baada ya wanachama hao kuwasili katika ofisi za CCM wilayani humo zilizopo eneo la maliasili Pasiansi, kwa lengo la kutaka kufahamu sababu za Maliki Hatibu kukatwa jina lake na kudaiwa kuwa si raia wa Tanzania licha ya kushinda kwa kura 720 dhidi ya kura 597 alizopata mshindi wa pili Steven Mashamba kwenye kura za maoni zilizofanyika Agosti mosi mwaka huu.
 
Askari polisi wakiwa na silaha na mabomu ya machozi walilazimika kuimarisha ulinzi katika eneo lote linalozunguka ofisi za chama hicho, huku baadhi ya wanachama wakichana kadi zao na wengine kwa hasira wakivua nguo na kubakia uchi huku wakijiapiza kuwa kamwe hawataondoka katika eneo hilo bila jina la Maliki Hatibu.
 
Katibu wa CCM wilayani Ilemela Acheni Maulid amezungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kutoa ufafanuzi kuhusu tuhuma zinazoelekezwa kwa mshindi huyo wa kura za maoni, Na pia mwandishi wa habari hii amewasiliana kwa njia ya simu na mgombea huyo Maliki Hatibu kwa lengo la kutaka kufahamu ukweli kuhusu uraia wake ambapo amesema ni raia wa Tanzania na alizaliwa mkoani Kigoma.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo