Indonesia imekua kwenye rekodi mbaya ya ajali za ndege huku ajali mbili za ndege zimeripotiwa ndani ya mwaka mmoja uliopita ikiwemo Indonesia Air ilianguka katika bahari ya Java ikitoka Sura Baya kuelekea Singapore na kuua watu wote 192.
Historia imerudi tena nchini humo baada ya ndege moja iliyobeba abiria 54 kupoteza mawasiliano na idara ya kituo cha udhibiti wa safari za ndege.
Maafisa wa idara ya uchukuzi wanasema kuwa ndege hiyo inayomilikiwa na kampuni yaTrigana Air ililikuwa ikielekea katika mji wa Oksibil Mashariki mwa jimbo la Papua kabla ya kutoweka.
Msemaji wa wizara hiyo amesema kuwa hatua za kuisaka ndege hiyo zimeanza na zinashirikisha mamlaka ya eneo hilo na kwamba hali mbaya ya hewa katika milima ya eneo hilo inaathiri utafutaji wa ndege hiyo.