Idadi ya wanaokufa kwa Kipindupindu yazidi kuongezeka jijini Dar es Salaam

Chalila Kibuda,Globu ya jamii
UGONJWA wa kipindupindu unazidi kusambaa katika manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi habari leo Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni,Aziz Msuya amesema watu waliofariki katika manispaa hiyo watatu.

Amesema idadi ya wagonjwa katika manispaa imezidi kuongezeka kutoka 34 hadi kufikia 43.

Amesema dalili za huo ni  homa kali ,kuharisha pamoja na kutapika na kuongeza kuwa mtu akifikia dalili hizo awahi katika kituo cha afya.

Aidha amesema kujiepusha na ugonjwa huo ni kuzingatia usafi wa vyakula ,maji pamoja na kunawa mikono kwa usafi wakati wa kula.

Msuya amesema watu waliokuwa wamelalazwa na ugonjwa huo watatu wamerusiwa.

Katika zahanati ya Mburahati wagonjwa wa kipindupindu waliolazwa ni  21.

Muuguzi Mkuu wa Zahanati hiyo, Nusra Kessy amesema kuwa wagonjwa hao wanaendelea kutibiwa katika zahanati hiyo.
  Usafi ukiendelea katika Zahanati ya Mburahati katika kukabiliana na Ugonjwa Kipindupindu mara baada ya Globu ya Jamii kutembelea kujionea hali halisi ya ugonjwa huo jijini Dar es Salaam.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo