Kwa mujibu wa Naibu katibu mkuu wa madereva (TADU), Rashidi Saleh aliwaeleza madereva hatima ya kamati ambayo imeundwa na Waziri Mkuu kusuluhisha kero za Madereva nchini.
‘Tarehe 13 /8 tulipo kwenda baada ya wao kusikia kuna tishio la mgomo,tulizani kwamba tunakwenda kujadili kwanini tunataka kugoma kwasababu tunazo kero zetu matokeo tulikutana na ajenda ya mizani ya vigwaza ,tukakutana na matatizo ya wamiliki, kamati kwenda Zambia kwenye ukaguzi wa mafuta, kamati kukagua spidi za magari na timetable ya Sumatra wiki ijayo.Naibu Katibu TADU’ – Rashidi Saleh
‘Kesho tutatoa tamko kwa waandishi wa habari kuhusu hatima ya madereva wa Tanzania,vyombo vyote vya habari kuanzia TV,Radio,Magazeti vitaonesha kwa hiyo kaeni karibu na vyombo vya habari’ -Rashid Saleh
‘Kuacha kuendesha sio mgomo si umepumzika,Nani kasema mgomo sisi atugomagi uwa tunajipa likizo vibarua uwa analikizo yake mwenyewe mpaka sasa sisi bado ni vibarua. Sisi tunataka tuweke semina atakama ya siku tatu maana na sisi tunahasira na ajali hivyo tutawaita walimu waje watufundishe na wale ambao wapo Tunduma nao wasivukea kwasababu awatapata mafunzo maana redio haziskiki nje ya nchi’ – Rashid Saleh