Katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF maalim Seif Sharif Hamad amesema umoja na mshikamano ndiyo utakaoleta ushindi wa kishindo ndani ya UKAWA hapo mwezi Octoba mwaka huu na kwamba hakuna mabadiliko yoyote yasiyokuwa na misuko suko hivyo amewataka wanachama wa CUF na wananchi kuwa watulivu kwani ukawa bado ni moja.
Maalim Seif ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akimkaribisha mgombea urais kupitia tiketi ya Chadema Mh Edward Lowasa ambaye ametembelea ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni ambapo mbali na kupongeza wanachama hao kubaki wamoja hata baada ya mwenyekiti wa chama hicho kujiuzulu wadhifa huo huku akiwataka kujitokeza kwa wingi kumsindikiza mgombea huyo kuchukuwa fomu ya kugombea urais jumatatu agost 10 mwaka huu.
Akizungumza na mamia ya wanachama wa CUF waliojitokeza kumpokea Mh Lowasa amesema mwanasisa yeyote shupavu na anayeipenda nchi yake hakati tamaa huku akimpongeza Maalim Seif kwa mapambano yake kisiasa ndani ya mfumo wa vyama vingi vya siasa bila uoga na kuongeza kuwa sera nzuri zenye usimamizi ndiyo zitakazowaondoa watanzania kwenye umaskini.
Mwenyekiti wa Chadema Mh Freeman Mbowe ambaye ameongozana na mgombea huyo amekiri UKAWA kukumbwa na dhoruba na misuko suko mingi ndani ya miezi nane lakini kwa umoja wao wameweza kuihimili hadi leo huku mwenyekiti wa NCCR-mageuzi Mh James Mbatia akiwataka wana UKAWA na watanzania wakiona uovu unatendeka waukemee na chuki yao wakaionyeshe kwenye sanduku la kura.
Naye mwanasheria wa Chadema Mh Tundu Lissu akatumia hadhara hiyo kutolea ufafanuzi uvumi aliyouita uzushi unaotembea kwenye mitandao ya kijamii juu ya mgombea urais kuwa hawezi kugombea kama hajawa mwanachama wa chama husika kwa miezi mitatu na hapa naeleza.