Dr Magufuli amewataka wananchi kuepuka viongozi wenye uchu wa madaraka.

Mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi Dr John Pombe Magufuli amewatahadharisha watanzania kuwaepuka kama ukoma viongozi wanaotafuta madaraka na mamlaka ya kuiongoza Tanzania kwa kuwa wana maslahi binafsi na hawatawajali wananchi wa kipato cha chini huku akitangaza mwisho wa wanafunzi hasa wa shule za msingi kukaa chini.

Akizungumza na mamia kwa maelfu ya wananchi wa wilaya ya mbarali mkoani Mbeya mgombea wa kiti cha urais Dr John Pombe Magufuli amewatahadharisha watanzania kuepuka mtindo wa kuwaweka madarakani viongozi mbalimbali kwa kuhongwa kwa kuwa iko siku viongozi hao watawageuka na kuwauza na kwamba hiyo ndio sababu kubwa ya Tanzania licha ya kuwa na rasilimali nyingi kushindwa kupiga hatua za kimaendeleo kwa kuwa viongozi wengi wanowekwa madarakani wanatumia fedha na hivyo wanapopata mamlaka hutumia muda wao mwingi kutafuta mbinu za kurejesha fedha hizo badala ya kuwaletea wananchi maendeleo.
 
Dr Magufuli ambaye amefanya mikutano ya hadhara katika maeneo ya Mbarali, Rungwe, makongorosi na chunya kwa nia ya kujinadi na kuomba ridhaa ya watanzania kuiongoza nchi huku akizungumzia matatizo mbalimbali na kuahidi endapo atapata ridhaa ya watanzania kuiongoza Tanzania mbali na wanafunzi kusoma bure bila ya kulipa karo kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne pia itakuwa mwisho kwa wananfunzi kukaa chini kwa kukosa madawati.
 
Nao baadhi ya wananchi katika maeneo alikofanya kampeni Dr John Pombe Magufuli wamesema kwa sasa Tanzania inahitaji rais mwadilifu atakayejali shida za watanzania hasa wa kipato cha chini na ambaye anamwogopa mungu ili nchi iweze kupiga hatua za kimaendeleo. 
 
Dr Magufuli anatarjiwa kuendelea na kampeni zake ambapo ijumaa ya August 27 anatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara katika jiji la Mbeya ambapo pia amejinadi kuwa serikai ijayo itakuwa ni serikali inayojali aina zote za jamii wakiwemo walemavu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo