Watu 9 wa Familia Moja Waliokufa kwa kuungua moto Wazikwa

Watu Tisa wa familia moja wakiwemo watoto watano wakazi wa Buguruni Malapa jijini Dar es salaam wamepoteza maisha majira ya saa tisa usiku baada ya nyumba yao kuteketea kwa moto unaodaiwa kusababishwa na hitilafu ya Umeme.

Baadhi ya jirani waliofika eneo hilo kwa ajili ya kutoa msaada wamesema walisikia vilio usiku huo na kuamka ili kuwahi kutoa msaada lakini walishindwa kutokana na moto kuzidiwa na moto uliokuwa ukiwaka kwa kasi huku mlango wa mbele kuingilia kushindwa kufunguka....

Mkuu wa mkoa wa dsm pamoja na kamanda wa polisi kanda maalum dsm CP  Suleiman Kova wamefika eneo la tukio na kupewa maelezo ya awali ya chanzo cha moto huo pamoja jitihada zilizofanywa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi bila mafanikio baada ya kinachosadikiwa kuwa mtungi wa gesi kulipuka na kusababisha watoa huduma kuingiwa na hofu.

Mamia ya watu walio na simanzi wamejitokeza katika hospitali ya taifa Muhimbili ambapo swala ya kuswalia maiti wote tisa zimefanyika kabla ya maziko.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amewafariji ndugu na jamaa wa familia na kuwaomba kuwa na subira huku serikali ikiahidi kuwa karibu nao kwa hali na mali kufuatia janga hayo.

Katika makaburi ya kisutu Mamia ya waombolezaji wameungana na ndugu na jamaa kushiriki katika mazishi huku wakiiomba serikali kuimarisha vikosi vya zimamoto ili viwe jirani na makazi ya watu.

Mmiliki wa nyumba hiyo Masoud Matar alikuwa kazini wakati wa tukio hilo linatokea ambapo watoto wake Abdallah miaka 10, aisha miaka 13, ahmed miaka 14,ashraf, ,10...pamoja na mkewe Samira juma miaka 27 wamepoteza maisha, Wengine waliofariki katika janag hilo ni Bi mdogo masoud miaka 80, samira haroun na mtoto wake mwenye umri wa miaka 17..


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo