Chama cha ACT – Wazalendo kimewaonya chama cha Demokrasia na Maendeleo kuacha kuwafanyia vurugu katika mikusanyiko yao pamoja na kushuka bedera za chama hicho.
Hayo yameelezwa na Katibu Mipango na Mikakati Habibu Mchange ambapo amedai kuwa chama cha Chadema kimevunja matawi baadhi ya maeneo nchini hivyo na kuwatia hasara kubwa.
Mchange amesema kama tabia hiyo ikiendelea basi ni wazi watawachukulia hatua za kisheria wapinzani wao hao.
Pia chama cha ACT kimetangaza rasmi kwamba kitaanza kampeni zake za kusaka urais,ubunge na madiwani siku ya agosti 30 katika viwanja vya Mbagala Zakhem – Jijini Dar es Salaam.