Chama cha Mapinduzi chapata msiba

Muasisi wa Tanu na baadaye CCM, Mzee Peter Kisumo amefariki dunia.
Mwanasiasa huyo mkongwe nchini ambaye aliwahi kushika nyadhifa kadhaa katika Serikali ya Awamu ya Kwanza, alifariki Dunia jana saa moja usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mtoto wa marehemu, Michael Kisumo alilithibitisha jana juu ya kifo cha baba yake akisema kilitokana na maradhi ya figo ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.
“Tulikuja hapa Muhimbili kwa ajili ya mzee kufanyiwa dialysis (usafishaji damu katika figo) sasa ikajitokeza complication (utata) akaanza kuharisha damu,” alisema.
Michael alisema baba yake alilazwa wodi ya kawaida juzi ili jana apatiwe tiba hiyo kabla ya hali yake kubadilika ghafla.
Daktari wake alipokuja leo (jana) na kumwangalia aliagiza atolewe wodi ya kawaida ahamishiwe ICU lakini ilipofika saa moja usiku akatutokaMichael.
Kifo cha mwanasiasa huyo kimekuja takribani mwezi mmoja tangu arejee kutoka India ambako amekuwa akienda mara kwa mara kuchunguzwa afya yake.
Hali ya ugonjwa wake huo ilifikia katika kiwango cha juu na kulazimika kufanyiwa uchujaji wa figo mara tatu kwa wiki kila Jumatatu, Jumatano na Ijumaa.
Kisumo aliwahi kuwa mmoja wa mameneja wa kampeni wa Rais Jakaya Kikwete mwaka 2005 akisimamia kanda ya kaskazini iliyojumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Tanga.
Mbali ya kuwa waziri, aliwahi pia kuwa mkuu wa mkoa na mdhamini wa CCM.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo