Chama cha Mapinduzi chamtoa hofu Dkt Magufuli

Chama cha mapinduzi CCM kupitia wenyeviti wa mikoa wa chama hicho, wameapa kukipigania chama hicho hadi hatua ya mwisho na kuwa hakuna chama mbadala cha kutatua matatizo ya wananchi zaidi ya CCM kwa kuwa vyama vingi vya kisiasa hapa nchini viko kwa ajili ya maslahi ya viongozi huku wananchi wakitakiwa kutafakari na kuwachambua wagombea ili kufahamu azma yao ya kusaka madaraka na kutofautisha wale wenye maslahi binafsi na wale wenye nia ya kuleta maendeleo nchini.
 
Mwenyekiti wa wenyeviti wa chama hicho Bwana Ramadhani Madabida ameyasema hayo mkoani Dodoma mara baada ya kumalizika kikao cha halmashauri kuu cha kupitia majina ya wagombea udiwani na ubunge na kuongeza kuwa kwa tathmini ya haraka wanaoondoka CCM kwa sasa ni wale walioshindwa kupata nafasi ndani ya chama hicho au majina yao kukatwa na vikao halali ndani ya chama hicho kikongwe nchini.
 
Awali mgombea wa nafasi ya urasi wa jamuhuri ya mungano wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi CCM, Dkt John Pombe Joseph Magufuli, amewaomba wenyeviti hao wa CCM wa mikoa nchini kuwa wamoja katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais wabunge na udiwani.
 
Katibu mkuu wa chama hicho komredi Abdulrahman kinana amewaeleza wenyeviti hao juu ya chama hicho kujipanga vizuri kwenye uchaguzi huu kwa kutumia njia ya anga, majini na nchi kavu kwa kuwa na ilani bora inayokidhi matakwa ya wananchi walio wengi, kuweka mgombea anayekubalika na wananchi, huku akiwasisitizia wenyeviti hao kuwa chama hicho, kimeaminika na watanzania wengi kwa mtu mmojammoja ama vikundi,hatua itakayopelekea chama hicho kuibuka na ushindi wa kishindo chini ya uratibu wa katibu mkuu mwenye uzoefu ndani ya chama cha mapinduzi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo