Wananchama na viongozi wa CCM waliohamia chama Chadema akiwemo aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Bw Laurence Masha wamesema uamuzi wa kukihama chama mapinduzi hautokani na tamaa ya madaraka kama inavyodaiwa bali wanajiepusha na matatizo yasiyo ya lazima likiwemo la ukiukwaji wa haki unaoendelea kujikita ndani ya chama hicho.
Wakizungumza na maelfu ya wananchi wa mkoa wa Mwanza walijitokeza kumpokea mgombea urasi wa umoa wa UKAWA kupitia chama Chadema Mh.Edward Lowasa viongozi hao wamewataka watanzania kujiepusha na matatizo yasiyo ya lazima likiwemo la kuendeleza siasa za chuki.