Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kimesema kwa sasa hakina muda wa kuzungumza kama mgombea wao wa urais Edward Lowassa na tuhuma alizokuwa nazo na badala yake wananchi wasuburi wakati wa kampeni ukifika
Hayo yamesemwa na makamu mwenyekiti wa CHADEMA taifa Prof Abdallah Safari wakati akizungumza leo katika kipindi cha siasa za siasa kinachorushwa na kituo cha EATV
"Hakuna haja ya kuongea sasa, kuna wakati wa kampeni unakuja sisi ndio tunajua tutazungumziaje hili suala la Lowassa kama tunamsafisha ama vipi" amesema Prof Safari
Amesema wananchi ndio wataamua wenyewe baada ya kupima ufafanuzi utakaotolewa kuhusu tuhuma zote za Lowassa na wao waamue