Chama cha wananchi CUF kimeahirisha mkutano wake na waandishi wa habari ulioitishwa na mwenyekiti wa chama hicho taifa Prof. Ibrahimu Lipumba
Taarifa za kuahirishwa mkutano huo zimetolewa na naibu katibu Mkuu Magdalena Sakaya amewaomba radhi waandishi wa habari waliofika kwenye makao makuu ya Chama hicho Buguruni jijini DSM ambapo zimeonekana kuzua hali ya sintofahamu
Amesema mkutano huo umeahirishwa na hawafahamu ni nini alichokuwa akizungumze Prof Lipumba lakini kwa hivi sasa Lipumba anazungumza na wazee wa chama hicho kwa kuwa wanataka kufahamu ni kitu gani angekwenda kukizungumza kabla hajakwenda kukizungumza
Katika tukio jingine mwandishi wa habari na mpiga picha wa magazeti ya UHURU Immanuel Ndege amejeruhiwa kwa kukatwa na feni kichwani katika ofsis hizo za CUF wakati akipiga picha kinachoendelea katika mkutano huo