Breaking News: Matokeo ya Uchaguzi CCM Udiwani na Ubunge kata ya Tandala Makete

Leo kulikuwa na upigaji kura ya maoni kuwapata wagombea wa Ubunge na udiwani katika majimbo na kata mbalimbali nchi nzima kupitia chama cha mapinduzi CCM

Yafuatayo ni matokeo ya uchaguzi huo kwa kata ya Tandala wilaya ya Makete mkoa wa Njombe kwa ngazi ya udiwani na Ubunge kama yalivyotolewa na msimamizi wa uchaguzi kata ya tandala Bw. Yusuph Kisimbilo Sanga

1. Udiwani
Walikuwepo wagombea wawili ambapo mtetezi wa nafasi hiyo Bw. Egnatio Mtawa amepata kura 675 dhidi ya mshindani wake Bw. Yusuph Ilomo aliyepata kura 79

2. Ubunge (kata ya Tandala tu)

Prof Norman Sigalla amepata kura 481, Dr. Binilith Mahenge anayetetea nafasi yake amepata kura 200, Boniki Mhami 36, Fabian Nking'wa 32, na Lufunyo Nkinda 11

Matokeo halisi ya ubunge bado yanakusanywa na yakikamilika utayapata hapa hapa


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo