Watu wanne wamezirai na kukimbizwa katika hospitali ya Nyahururu, Kenya baada ya kuzidiwa kwa kukosa pombe.
Kulingana na madaktari katika hospitali hiyo, wanaume hao walilazwa baada ya juhudi za kuwarejeshea fahamu kwa kuwanywesha maziwa kugonga mwamba.
Ofisa matibabu katika hospitali hiyo ambaye alikataa jina lake kutajwa alisema wanaume hao walianguka na kukosa fahamu baada ya kukosa pombe walioachishwa gafla.
“Kawaida mtu akiwa na mazoea ya kunywa pombe kisha kumwachisha ghafla mwili huhisi kukosekana kwa kiungo muhimu”.
Alisema kwa sasa watu hao wanaendelea vizuri na matibabu na kufuatia tukio hilo walevi waliokuwa kwenye kampeni ya kuacha ulevi wameishutuma Serikali kwa hatua ya kuwalazimisha kuacha pombe gafla.
Wakazi wengi wa eneo hilo walisema hawawezi kufanya kazi bila kunywa pombe kwa kuwa inawasaidia kuwaongezea ari ya kujituma
