Ujio wa Lowassa Chadema Dodoma yazizima

SHUGHULI zimesimama katika mji wa Dodoma kwa muda wote ambao Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeutumia kumtambulisha Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kujiunga na Chama hicho.

Aidha, vikundi vikundi vya watu katika maeneo mbalimbali ambapo kulikuwa na runinga wakishangilia na kufurahia ambao umefanywa na Lowassa kwa kujiunga katika Chadema na kuendeleza mapambano na Ukawa.
Baada ya Lowassa kutangaza kuwa amejiunga rasmi na chama hicho makundi ya vijana pamoja na watu wazima walionesha kupiga kelele za shangwe huku wakisema mwisho wa CCM umefika.
Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Kanisa la Endtime Harvest na Katibu wa Umoja wa Madhehebu ya Kikristo mkoa wa Dodoma, Dk Elia Mauza akizungumza na Mwanahalisi Online amesema kitendo cha Lowassa kuhamia upinzania ni ujasiri wa hali ya juu na ni mpango wa Mungu.
Amesema kati ya viongozi walioonesha ujasiri ndani ya serikali ya CCM alikuwa ni Lowassa ambaye alikuwa mkweli na mbunifu katika kuhakikisha maisha ya watanzania wainuka kimapato.
Askofu Dk Mauza aliwataka watanzania wakumbuke kuwa mwenye maono ya kuazisha shule za kata alikuwa Lowassa lakini baada ya kufanyiwa fitina na kujiuzulu uwaziri mkuu kwa faida ya serikali hadi sasa shule hizo zimedorora .
Hata hivyo amesema kitendo cha uongozi wa Chadema kwa kushirikiana na Ukawa kumkaribisha kada hiyo kujiunga na wao ni dalili za ukomavu wa kisiasa ambazo zinalenga kuwapatia ukombozi watanzania wanyonge.
Kwa upande wao wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kwa Machinga waliliambia gazeti hili kuwa kuijiunga kwa Lowassa Ukawa ni dalili za ukombozi kwa watanzania wanyonge.
Mmoja wa wasomi wa Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM ambaye hakutaka jina lake litajwe aliliambia gazeti hili kuwa kitendo cha kuingia upinzani ni ishara tosha ya kuiondoa CCM madarakani.
“Hata huyu Dk .Magufuli ambaye anashangiliwa kuwa ni jembe hakuna jambo lolote ambalo anaweza kulifanya kuwa jipya ndani ya kutokana na mfumo ambao hupo kwa sasa mfumo wa CCM umejaa ufisadi na kulindana kwa wala rushwa.
chanzo:mwanahalisionline


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo