Sababu za wanafunzi kushindwa kusoma na kuandika zawekwa wazi

Moja kati ya sababu zinazotajwa kuchangia wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika wilaya ya uyui mkoani Tabora kushindwa kujua kusoma na kuandika inatokana na kutokuwepo kwa vitabu vya masomo mbalimbali vikiwemo vya ziada na  kiada,hatua ambayo pia imewaondolea moyo wa kujisomea kwa wanafunzi wanaojua  kusoma.

Akizungumza kwa niaba ya Afisa Elimu wilaya ya Uyui wakati wa hafla fupi ya  kukabidhi Msaada wa vitabu vilivyotolewa na Mradi wa vijiji vya Milenia Mbola,Afisa Elimu Vielelezo Bw.Cassian Luoga,amesema bado kumekuwa na tatizo la upungufu wa vitabu katika shule za msingi na Sekondari Wilayani Uyui na hivyo  kukwamisha kasi ya maendeleo  ya Sekta  ya Elimu mashuleni.
 
Aidha Bw.Luoga pamoja na kutoa shukrani kwa Mradi wa vijiji vya Milenia mbola  kwa kutoa  msaada  huo wa vitabu hivyo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi  milioni 23,amewataka Wazazi wa wanafunzi kujenga tabia ya kushirikiana na Serikali kuchangia maendeleo katika sekta ya elimu,huku Mratibu wa Elimu wa Mradi wa vijiji vya Milenia Mbola Bw.Nemes Temba akitaja malengo mahususi ya msaada huo katika kuinua kiwango cha elimu kwa wanafunzi.
 
Kwaupande wake Mwalimu mkuu wa moja kati ya Shule  nne  zilizopata msaada  huo  wa vitabu,Shule ya Msingi Madaha Bi.Catherine Mmbando amesema msaada huo  umekuja wakati muafaka ambapo Shule hizo hazina vitabu vya kutosha kukidhi  mahitaji ya kufundishia 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo