Picha za msanii Bongo akijifungua zaanikwa!

Imelda Mtema
MSANII zao la Kundi la Sanaa la Kaole, Mwasiti Mohamed ‘Sishi’ zimeanikwa katika mtandao wa kijamii wa Instagram zikimuonesha wakati akijifungua akiwa kwenye uchungu mkali.

Sishi ambaye kwa sasa anaishi Ufaransa, katika picha hizo alionekana kusaidiwa na mama aliyejulikana kwa jina la Bi. Rukia, ambaye ndiye aliyempeleka nchini humo, huku mashabiki walioziona picha hizo baadhi wakimuonea huruma huku wengine wakishangazwa na kitendo hicho wakidai hakikuwa cha kimaadili.

Gazeti moja la global publishers lilipowasiliana na Bi. Rukia kwa njia ya mtandao wa WhatsApp alisema; “Mbona hakuna cha ajabu jamani? Ile ni kumbukumbu tu na huku ni vitu vya kawaida mno, sasa watu wakichukulia kama ishu kubwa mimi nitashangaa sana kwa kweli.”


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo