Bw. Jackson Mbogela mgombea Ubunge jimbo la Makete 2015.
Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema wilaya ya Makete kimefanya uchaguzi wa kumpata mgombea atakayepeperusha bendera ya chama hicho kuwania Ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu
Uchaguzi huo uliokuwa na wagombea 7, umemalizika wa Bw. Jackson Mbogela kuibuka mshindi kwa kupata kura 143, Ahadi Mtweve 77, Oddo Chaula 09, Emmanuel Meck 08, Adson Solomon Sanga 02, Benjamin Bukuku 01 na Abihud Mwandikilu hakupata kura hata moja
Kwa matokeo hayo Bw. Jackson Mbogela ameibuka mshindi kwa kutangazwa na msimamizi wa uchaguzi huo Bi Beatrice Kyando
Katika mahojiano na mwandishi wetu Bw. Mbogela amesema wanamakete wategemee mabadiliko kwa kuwa wao kama CHADEMA wamejipanga vizuri kuhakikisha wanashinda katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba Mwaka huu
Uchaguzi huo umefanyika Julai 22 katika ukumbi wa shule ya sekondari Iwawa katika mji mdogo wa Iwawa wilayani Makete mkoani Njombe
Hoi hoi vifijo na nderemo baada ya ushindi wa Mbogela.