Inasikitisha: Mmiliki wa mabasi ya J4 adaiwa kupiga watu wawili kwa risasi na kuwaua


Waliouawa ni Ali Mohamedi na Claudia Sikarwanda. 

Star TV imeripoti kuwa mmiliki wa mabasi ya J4 Bw.Juma Mahende anadaiwa kuwapiga wafanyabiashara wenzake wawili kwa risasi mbele ya ofisi yake na kufariki papohapo.

Tukio hili la Hatari limetokea Mwanza.

Jeshi la polisi limemkamata na kumtia ndani mtuhumiwa huyo wa mauaji. Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza Bw.Mkumbo amethibitisha kutokea kwa tukio hili. 

Ndugu wa marehemu wanasema jamaa waliouawa na muuaji walikuwa wanadaiana 25 Milion. Inashangaza na kuhudhunisha kama haya yanaweza kutokea Tanzania.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo