Haya mashindano ya kung'atwa na Mbu balaa

Mbu wanajulikana kwa kuwa adui namba moja wa binadamu kutokana na kusababisha malaria… pengine hili lililotokea Russia linaweza kukushangaza na kukushtua kidogo.
Katika mji wa Perm wameamua kila mwaka kusherehekea tamasha la kipekee la mashindano ya kuchagua msichana mrembo zaidi ambapo watashindanishwa kwa kuvaa nguo fupi na atakayekuwa na alama nyingi za kuumwa na mbu baada ya kusimama kwa dakika zipatazo 20 katika eneo lenye mbu wengi ataibuka mshindi.
Shindano limeandaliwa na Natalya Paramonova litasimamiwa na majaji wakiwemo madaktari ambao watakagua miili yao na msichana atakayekuwa na alama nyingi za kuumwa na mbu ndiye atakuwa mshindi.
Shindano hilo pia liliwahi kufanyika mwaka 2013 huku mshindi akiwa na alama za kuumwa na mbu mara 100.
Mbali na shindano hilo pia lipo la kushika mbu akiwa hai.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo