CCM yatangaza kumfikisha mahakamani Mh. Wenje

Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje atafikishwa mahakamani na chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza wakati wowote akituhumiwa kuwaibia wananchi wa jimbo hilo milioni 75 za mfuko wa jimboni humo.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Katibu mkuu wa CCM Mkoa Miraji Mtuturu wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika soko la Igogo, Nyamagana.
Alisema CCM itaweka wakili ili Mbunge huyo awaeleze wananchi zilipo milioni 75 alizochangisha kwa ajili ya kusaidia kuboresha mfuko wa elimu jimboni kwake, lakini akazitumia kwa mafufaa na maslahi yake na familia yake.
Alidai Wenje alianzisha mfuko wa elimu ambapo Rais Kikwete alichangia milioni 10, Zittona wageni wengine walichangia milioni 8 na Raila Odinga alichangia dola za Marekani 6,000.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo