Mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongela amesema hayo mara baada ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapigakura katika kituo cha uwanja wa ndege mjini Bukoba ambapo amewataka wahamiaji haramu waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kinyume na sheria kujisalimisha mara moja kabla sheria haija chukua mkondo wake.
Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongela amesema Tanzania sio shamba la bibi kuwa kila mtu anaweza kufanya anachotaka kinyume na taratibu za nchi nakwamba serikali haiwezi kuwavumilia raia wanaoingia nchini kunyume na sheria nakujificha kwa kivuli cha vyama vya siasa huku akiwataka wananchi kutosita katika kuwafichua wahamiaji haramu wanaoshirika katika zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Hali hiyo imejitokeza kufuatia baadhi ya vituo vya kuandikisha watu katika daftari la kudumu la wapiga kura kubainika kuwa na wimbi la wahamiaji haramu na hasa katika wilaya ya Kyrwa ambayo ikopembezoni mwa nchi ambayo pia imepakana na nchi jirani za Rwanda na Uganda.