Akihutubia mamia ya wananchi katika mji wa vawa wilayani Mbozi, katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo, Chadema, Dk. Wilbrod Slaa amesema kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini wako hatarini kupoteza haki yao ya kidemokrasia ya kupiga kura, kwa kuwa baadhi yao wamejiandikisha kwenye vituo wakati wakiwa vyuoni, lakini wakati wa kupiga kura vyuo hivyo vtakuwa vimefungwa na wanafunzi watakuwa majumbani mwao.
Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Mbeya, Joseph Mwachembe maarufu kwa jina la china amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya kuandikishia wapiga kura ili wakajiandikishe, huku pia akiiomba tume ya taifa ya uchaguzi kuongeza mashine za uandikishaji kwenye vituo ambavyo vina msongamano mkubwa wa wananchi wanaokwenda kujiandikisha.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chadema kanda ya nyanda za juu kusini, mchngaji Dk. Steven Simon Kimondo amesema kuwa monyoko mkubwa wa maadili ndio ambao umeliingiza taifa kwenye matatizo makubwa ikiwemo ubadhirifu wa mali za umma.