Wakizungumza na waandishi wa habari bungeni mjini Dodoma wabunge wa chama cha wananchi-CUF- wamesema watu zaidi ya 400 wamenyimwa kujiandikisha katika daftari la wapiga kura katika wilaya ya mkoani, jimbo la Kiwani na, jimbo la Mkanyageni pamoja na wengine kutoka Unguja kutokana vikwazo mbalimbali ikiweo kutopewa vitambulisho vya mzanzibar mkazi.
Baadhi ya wabunge wamewatuhumu baadhi ya wakuu wa wilaya na mikoa visiwani Zanzibar kwa kukabidhiwa jukumu la kuhakikisha baadhi ya wanachama na wafuasi wa CUF haingizwi majina yao katika daftari ya wapiga kura lengo likiwa ni kupunguza kura zao katika uchaguzi mkuu baada ya kugundua chama cha wananchi CUF kinawananchi wengi.
Wakati hayo yakijitokeza huko Zanzibar, kwa upande wa Tanzania bara baadhi ya wabunge wa majimbo yaliyo ndani ya mkoa wa Kilimanjaro wamemtaka rais Jakaya Kikwete kumuwajibisha mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kwa tuhuma za kutumia madaraka yake vibaya, pamoja na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa kumchunguza na watendaji wake dhidi ya tuhuma za kutumia fedha za umma katika kuanzisha kampuni binafsi.