Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu linamshikilia Mwenyekiti wa kijiji cha Bukigi kupitia chama cha Mapinduzi CCM kwa kosa la kukutwa na viungo vya binadamu likiwemo fuvu la kichwa na mifupa.
Mtuhumiwa huyo ambaye pia ni mganga wa jadi alikamatwa nyumbani kwake baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa amewahifadhi majambazi wakisubiri kupangwa waendelee na uhalifu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Gemin Mushy alisema tukio hilo lilitokea Mei 9 na walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema.
Alisema kuwa upepelezi unaendelea kubaini iwapo kweli viungo hivyo ni vya binadamu na kama kuna watu wengine wanahusika.