Kuna stori kutoka Nigeria kwenye mji wa Anambra ambapo Mgawaha mmoja umedaiwa kuwauzia wateja wao nyama za binadamu tena kwa bei kubwa tofauti na bei nyingine.
Inasemekana Polisi walipewa taarifa hizo na kuamua kufanya uchunguzi na ndipo walipovamia mgahawa huo na kukuta vichwa viwili vya binadamu vikiwa ndani ya mfuko na tayari vimekatwa.
Mmoja wa watu waliopokea kwa mshtuko mkubwa taarifa hizo ni mchungaji mmoja ambaye aligundua amekula nyama isiyo ya kawaida na kuwa wa kwanza kuwataarifu Polisi ambao walifika na kubaini kuwepo kwa uuzaji huo.
Kwa sasa mgahawa huo umefungwa na wahusika 11 wanashikiliwa na Polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.