Kamati ya Bunge ya PAC imeagiza Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Mafutaa Mohamed kuondolewa Hotelini ambako amekaa tangu alipoteuliwa ambapo wamedai anaiongezea gharama Serikali.
Kaimu Mwenyekiti wa PAC, Ismail Rage amesema Mkuu huyo wa Wilaya ikifika May 31 itakuwa siku yake ya mwisho kukaa Hotelini hapo, ambapo amemtaka Katibu Tawala wa Mkoa kuangallia namna ya kumalizia ujenzi wa nyumba ya DC huyo.
Mhasibu wa Mkoa alipohojiwa na Kamati hiyo kuhusu gharama inayotumika kulipia Hoteli hiyo alijibu kwa kigugumizi kwamba wanalipia Tshs. 80,000/- kwa siku kutoka kwenye mfuko mwingine wa Wilaya hiyo.
Mkuu huyo wa Wilaya amekaa kwa miezi miwili Hotelini tangu alipoteuliwa kutokana na nyumba yake kutokamilika kujengwa.