Ikulu ya Tanzania sio mahali pa kuishi wagonjwa na watu waliochoka kama .......!!!!

Ikulu ya Tanzania sio mahali pa kuishi wagonjwa na watu waliochoka, bali ni kwa ajili ya viongozi makini na shupavu na wenye uwezo wa kuliongoza Taifa.
Imeelezwa kuwa viongozi waliochoka kama katibu wa Chadema Wilbroad Slaa ambaye amekuwa akipigiwa chapuo kuwania Urais hana sifa za kuishi ikulu.
Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde alisema  viongozi wa Chadema akiwemo muasisi wake Edwin Mtei wamechoka na licha ya kuchoka pia wamekuwa tegemeo ndani ya CHADEMA na ndio sababu wamekuwa wakipigiwa upatu kuingia ikulu.
Lusinde alikiri kuwa Serikali ya CCM imechoka kutokana na kufanya kazi nyingi za kuwatumikia wananchi wake kwa kutumia akili nyingi,maarifa na nguvu kwa lengo la kuhakikisha wanaishi katika maisha mazuri.
Alisema Serikali imekuwa ikitekeleza mambo mengi ya maendeleo kwa wananchi wake huku ikitimiza ahadi zote ilizoahidi katika ilani ya Uchaguzi tofauti na wapinzani.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo