Mkazi wa kijiji cha Ndelete, Kiteto Saria Kidali amefariki dunia baada ya kunyongwa na shuka alilokua amejifunika wakati anaendesha pikipiki.
Tukio hilo la aina yake lilitokea jana asubuhi wakati Kidali alipokuwa akitok,ea shambani kwake ambapo shuka ya mwendesha pikipiki huyo ilinasa kwenye tairi ya nyuma na kisha kumbana shingo hadi alipopoteza maisha na kudondoka chini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Christopher Fuime alithibitisha kutokea kwa kifo hicho.
Mashuhuda walisema walipata taarifa kutoka kwa abiria mmoja wa basi aliyekuwa akitokea Kiteto kwenda Arusha ambaye aliuona mwili wa mtu huyo ukiwa chini.