Diamond, na Ali Kiba wachuana Tuzo za Watu



WANAMUZIKI mahiri wa muziki wa Bongo fleva nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ na Ali Kiba, ni miongoni mwa wasanii wanaochuana katika Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume katika Tuzo za Watu 2015.
 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Bongo 5 Media Group, inayoratibu tuzo hizo, Nancy Sumari, wasanii wengine walio katika kipengele hicho ni Elias Barnaba, Ommy Dimpoz na Jux.
 
Katika kipengele cha msanii bora wa kike wanaochuana ni Lady Jaydee, Linah, Mwasiti, Shilole na Vanessa Mdee.
 
Filamu ya Chausiku, Kigodoro, Madam, Mshale wa Kifo na Sunshine zinashindana kwenye kipengele cha filamu zinazopendwa.
 
Msanii JB na Ray, wanachuana katika kipengele cha mwongozaji bora wa filamu sambamba na Leah Mwendamseke, Timothy Conrad na William Mtitu.
 
Alisema Jumamosi yatatangazwa majina ya tano bora na Mei 8 mwaka huu yatatangazwa majina ya waliotinga tatu bora ambapo fainali itafanyika Mei 22.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo