WANAFUNZI WA VYUO VIKUU IRINGA WAFURIKA HOSPITALI YA RUFAA, KISA DAMU

Mamia ya wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani Iringa leo wamefika katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa kuchagia damu ili kuongeza upatikanaji wa damu salama kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu ambao wamelazwa katika hospitali hiyo.

Wanafunzi hao kutoka chuo kikuu cha kikatoliki cha RUA, chuo kikuu cha Iringa, chuo kikuu cha elimu Mkwawa na chuo cha maendeleo ya jamii CDTI  wamesema wamefika hospitalini hapo kujitolea damu kama sadaka lakini pia kuunga mkono utekelezaji wa mpango wataifa damu salama.
 
Pamoja na kujitolea damu na kufanya shughuli za usafi katika hospitali hiyo, wanafunzi hao pia wamezungumzia mustakabali wa taifa hasa wakati huu ambao nchi inakwenda kufanya uchaguzi mkuu wa rais wabunge na madiwani ambapo wamesema mgombea urais wanayemkubali kwa ubora, uchapakazi na uadilifu ambaye wapotayari kumuunga mkono kipindi atakapotangaza nia ya kugombea urais ni waziri mkuu mstaafu Edward Ngoyai Lowassa.
 
Wanafunzi hao wamesema wakati umefika ambapo vijana wanataka kuyaishi mabadiliko na kusisitiza kuwa zama za kuchaguliwa viongozi umepitwa na wakati kwasababu wananchi ndiyo wenye mamlaka ya kuchagua kiongozi anayewafaa katika kutetea maslahi ya taifa na kuboresha maisha yao kiuchumi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo