MASIKINI FAMILIA HII YAFANYIWA KITU MBAYA HUKO ARUMERU

Wananchi wa familia saba za kijiji cha Sakila kilichopo kata ya kikatiti wilayani Arumeru mkoani Arusha wanalala nje na watoto wao huku  wakikabiliwa na njaa kali baada ya watu wanaodai kutumwa na serikali ya kijiji kuvunja nyumba zao na kufyeka migomba yao.

Wakizungumza nasi wananchi hao wanaodai kuwa wameishi maeneo hayo kwa zaidi ya miaka 30 wamesema wanashangazwa na viongozi wa kijiji hicho kutoa baraka za kuvunja kwa nyumba zao kwa kisingizio kwamba wao ni wavamizi.
 
Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw Richard Mbise amesema hatua hiyo imekuja baada ya mahakama kuthibitisha kuwa wananchi hao walivamia eneo hilo na walikiuka taratibu.
 
Hata hivyo baadhi ya viongozi wastaafu wa vijiji vya kata hiyo pamoja na kukiri kuwepo kwa mgogoro huo wamesema hatua ya zinazochukuliwa kuutatua zikiwemo za kuvuja  nyumba na kukata migomba sio sahihi.
 
Tatizo la migogoro ya ardhi katika wilaya ya Arumeru ambalo kwa sasa linaelekea kuwa sugu limeendelea kuwaathiri wananchi wa huku   baadhi ya viongozi wakiwemo wa kisiasa wakilitumia kama ajenda za kutafuta maslahi yao jambo ambalo lisipodhibitiwa linaweza kuleta  maafa makubwa.

Credits:ITV


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo