TAARIFA ZA HIVI PUNDE: RAIA WATEMBEZA KICHAPO KWA POLISI MKOANI MOROGORO

Image result for breaking news
Askari  wa Jeshi LA polisi Morogoro waliokua wakitumia pikipiki no PT 823 Mali ya jeshi hilo wamewekwa chini ya ulinzi na raia eneo LA Mindu na raia wamemjeruhi vibaya mmoja wao aitwaye Ramadhani.
Chanzo cha sakata hili ni ajali ya pikipiki waliokua wakiifukuza ambapo ilimshinda dereva bodaboda na kuingia kwenye lori.  Ndipo raia walipoanza kuwatuhumu polisi hao kuwa ni chanzo cha ajali na polisi waliamua kufyatua risasi hewani.

Hali ikawa tofauti, baadala ya raia kutawanyika waliongezeka na kuwazidi nguvu askari.

Cha kushangaza raia wamempiga kwa mawe askari mmoja na mwingine walimwambia yeye hana makosa. 

Aliyejeruhiwa ni yule anaedaiwa kusababisha kuumia vibaya dereva bodaboda Ali Zona muuza magazeti katika harakati za maandamano ya CHADEMA 2011.
NB:::TAARIFA HIZI BADO HAZIJATHIBITISHWA NA JESHI LA POLISI
CHANZO-FUNGUKALIVE


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo