Mkurugenzi wa mamlaka ya usafiri na nchi kavu na majini SUMATRA Gilliard Ngewe ameyasem ahayo mkoani Morogoro wakati akizungumza na wakuu wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kutoka mikoa yote nchini pamoja wa maofsa wa SUMATRA na maofsa wateule wa halimashauri ambapo amesema siku hadi siku ajali za barabarani zimekuwa tishio na zinajenga hofu kwa abiria ambapo amezitaka mamlaka husika kuhakikisha zinakuwa na mpango madhubuti kwa ajili ya kupambana na ajali hizo vinginevyo hakuna haja ya kuw ana vitengo hivyo.
Mkuu wa kikosi cha usalama bara barani Mohamed Mpinga akitoa taarifa kuhusu hali ya ajali nchini anasema ajali nyingi zimetokana na makosa ya kibinadamu ambayo yamejumuhisha uzembe wa madereva matumizi mabovu ya barabara ambapo amesema jeshi la polisi litaendelea kujipanga na kutumia mbinu mbalimbali kuhakikisha ajali zinamalizika.
Katibu mkuu TAMISEMI Jumanne Sagini amesema SUMATRA na halmashauri nchini zimefnaya makubalino kutizama upya matumzi ya pikipiki ambapo pamoja na kutoa huduma za usafiri zinatumika vibaya kwa matukio ya uhalifu.