MWANAUME AJIUA KWA KUNYWA SUMU KISA MKEWE KAMPAKULIA UGALI KIDUCHU

blog_nyamachoma_cMwanaume mmoja katika kijiji cha Migosi, Kaunti ya Siaya, nchini Kenya amejiua kwa kunywa sumu baada ya kugombana na mkewe kwa kile alichodai kuwa alimpakulia ugali mdogo.
Mwanaume huyo  Samuel Abuya, ambaye ni baba wa watoto kumi, alianza kugombana na mke wake kuhusu chakula muda mfupi baada ya kufika nyumbani akiwa amelewa.
Mtoto wake wa kiume David Ouma, amesema baba yake aliwafukuza nyumbani baada ya mama yake kumpakulia ugali na kuanza kulalamika kuwa ni mdogo na kutishia kujiua, baada ya kufukuzwa walikimbilia kwa mjomba wao anayeishi jirani, lakini aliwafuata  na kuendelea kugombana ndipo mama yake alipomuuliza kwa nini analalamika chakula kidogo wakati haachi hela ya chakula maneno yaliyomkasirisha na kuondoka huku akitishia kujiua.
Waliporudi nyumbani saa tano usiku walimkuta baba yao ameanguka chini akijigalagaza kwa maumivu, pembeni yake kukiwa na chupa yenye dawa ya kuulia mchwa, walijaribu kuokoa maisha yake kwa kumnywesha maziwa lakini hayakumsaidia akafariki.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo