KATONI FEKI ZA MAJI ZIPATAZO 574 ZAKAMATWA HUKO MUSOMA MARA

Jumla  ya katoni 574 ya maji ya kunywa kutoka kampuni mbalimbali nchini kenya yenye thamani ya shilingi milioni 3,444,000 ambayo yadaiwa kuingizwa nchini kinyemela na bila kuthibitishwa na mamlaka ya chakula na dawa TFDA na vibali wala nembo  ya shirika la viwango nchini (TBS)  yakamatwa na  kuteketezwa.

Akizunguza wakati wa zoezi la uteketezaji wa maji hayo ambao umefanyika katika eneo la Nyabange  nje kidogo ya  manispaa ya musoma, meneja  msaidizi usimamiaji madeni na kodi za ndani wa TRA Bw Ernest Nkangaza,amesema kuwa maji hayo ya aina mbalimbali kutoka nchi hiyo jirani,yameingizwa nchini kwa njia za panya kati ya machi 9 na april 9 mwaka huu,na kusambazwa katika miji ya tarime na Musoma.
 
Naye afisa afya mkoa wa mara Bw.Bumija Mhando,amesema maji hayo kiafya si mazuri kwani  yamegunduliwa kuwa ni maji ya kisima,ambayo ukaguzi wake haufahamiki na hivyo usalama wake  unatia mashaka makubwa huku yakiwa na bei ndogo ukilinganisha na makampuni mengini. 
 
Zoezi hilo la uteketezaji limefanywa na mamlaka ya mapato tanzania TRA Mkoa na idara ya afya  likisimamiwa na maafisa kutoka jeshi la polisi na usalama wa taifa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo