KABURI LILILOBOMOLEWA NA WEZI NA KUIBA NGUO ZA MAREHEMU LAJENGWA UPYA HUKO PWANI

Hii ishu inahusiana na tukio ambalo liliripotiwa kwenye vyombo vya habari ikiwemo Magazeti kuiandika sana.. ilishtua wengi, hata mimi iinishtua pia.. marehemu amefariki, ndugu wamefanya mazishi.. siku chache baadae wakaja watu wasiofahamika wakafukua kaburi na kuiba nguo mabegi mawili ambazo alizikwa nazo marehemu.
Hiyo picha hapo juu ni.. ndugu waliamua kulijenga upya baada ya wezi hao kubomoa na kuiba vilivyokuwemo ndani.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limethibitisha tukio hilo, wanawatafuta waliovunja kaburi hilo na kufanya uhalifu wa kuiba nguo na vitu vingine alivyozikwa navyo.

Shuhuda mmoja amesema walikuta kaburi limechimbuliwa, nguo zimetolewa na nyingine walikuta zimetupwa vichakani ikabidi wazichome moto.



JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo