Jeshi la polisi mkoani Shinyanga limewakamata wahamiaji haramu saba

Jeshi la polisi mkoani shinyanga limewakamata wahamiaji haramu saba katika matukio mawili tofauti wakiwa wanasafiri kutoka mwanza kuelekea DARI-ES-SALAAM kwa lengo la kwenda AFRICA KUSINI ambapo watanzania wawili wamekamatwa wakiwasafirisha wahamiaji hao haramu.


Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Bw. Justus Kamugisha amesema jeshi la polisi mkoa wa shinyanga limeanzisha operesheni kabambe ya kubaini na kuwakamata wahamiaji haramu wote na amewataka watanzania kuacha tabia ya kujihusisha na vitendo vya kuwahifadhi na kuwasafirisha watu hao na atakayekamatwa atafikishwa mahakamani na sheria itachukua mkondo wake.
 
watanzania wanaotuhumiwa kuwasafirisha wahamiaji hao haramu wamesema wao wametumwa kuwachukua watu hao mkoani mwanza na kuwafikisha katika mji wa kahama ambapo mtu mwingine atawachukua na kuwapeleka AFRICA KUSINI kupitia DAR-ES-SALAAM huku wahamiaji hao haramu wakidai kuwa wanasafiri kwenda AFRICA  KUSINI kutafuta maisha mazuri kwakua nchini kwao hali ya maisha ni duni.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo