Matukio ya mauaji ya watu wenye ulemavu ya ngozi yanaendelea kujitokeza nchini, ni wiki moja baada ya mtoto mmoja Yohana Bahati kuuawa Geita na watu wasiofahamika na leo kuna mlemavu mwingine ameripotiwa kukatwa mkono huko Sumbawanga.
Leo kwenye Power Breakfast Clouds FM, kulikuwa na mazungumzo na Mkurugenzi wa shirika linalotetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi la Under The Same Sun, Vicky Ntetema, amezungumzia jinsi ukatili huo unavyofanyika;
“Watu
ambao wanataka madini ule mguu wanasema kwamba unakuwa kama ni chombo
cha kuangalia madini yako wapi katika mwamba.. wanachokifanya ni kwamba
huu mguu unapelekwa katika eneo na kuna kelele ambazo zinatokea
wanazozisema wao kama vile kelele za kwenye redio wakati unatafuta
stesheni, kwa hiyo iyo kelele inapotokea ndipo ambapo mganga anawaambia
kwamba anze kuchimba“
Anaweza
kuambiwa achukue damu ambayo awe amekuja nayo au ni mganga kampatia
lakini pia ni damu ya binadamu, lazima kafara ya binadamu itolewe ile
damu sasa mganga anasema kwamba anaimwaga katika eneo moja halafu ule
mchuruziko wa damu ndio unaofuatwa pale ambapo hiyo damu itatuama katika
huo mchuruziko basi ndipo hapo huyu mtu wa madini ataambiwa kwamba anza
kuchimba katika eneo hili“
“..wakati
mwingine wanasema kwamba wanapoishiwa viungo wanawaomba wenzao.. kuna
muungano wa waganga wa kienyeji ambao wanatumia viungo vya watu wenye Albinism
anapoishiwa hapa anamuomba mwenzake Kijiji cha pili au kama sio Kijiji
cha pili anakwenda hata nchi jirani, hayo yote ni maneno yanayosemwa na
waganga wenyewe “– Vicky Ntetema.