Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Somanda Wilayani bariadi Janeth Mazigi
(28) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bariadi kwa makosa manne
(4) aliyoyatenda dhidi ya mtumishi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kwa
kile kinachosadikiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Hakimu huyo
inadaiwa kuwa alitumia wadhifa alionao kumteka mtumishi huyo (jina
linahifadhiwa) na kumnyanyasa kijinsia kinyume na sheria ya kanuni ya
Adhabu sura ya 16.
Akisomewa mashtaka hayo na Wakili wa Serikali
Mfawidhi Mkoani hapa Yamiko Mlekano mbele ya hakimu Mfawithi mahakama ya
wilaya Bariadi Aidan Mwilapwa wakili huyo alisema kuwa mshitakiwa
anatuhumiwa kwa kosa la wizi, utekeji, unyanyasaji, pamoja na kukutwa na
picha utupu.
Mlekano aliieleza mahakama kuwa mnamo tarehe
3/03/2015 mshtakiwa pamoja na askari polisi wa kike walimteka Mtumishi
huyo ofisini kwake kinyume na matakwa yake na kumpeleka nyumbani kwa
mshitakiwa Kidinda Bariadi Mjini kinyume na kifungu namba 133 cha kanuni
ya adhabu sura ya 16.
Kosa la pili la unyanyasaji wa kijinsia,
ilidaiwa kuwa katika tarehe hiyo hiyo majira ya saa 3 asubuhi nyumbani
kwa Mshtakiwa , alimpiga picha za utupu mtumishi huyo kwa kutumia
simu yake kwa lengo la kumdhalilisha na kumtolea maneno ya kashfa.
Kosa
la tatu kukutwa na picha za udhalilishaji, mshitakiwa ilidaiwa terehe
hiyo hiyo majira ya saa 3 asubuhi nyumbani kwa mshitakiwa alikutwa na
picha za utupu zilizokuwa katika simu yake alizokuwa amempiga mtumishi
huyo akiwa uchi kwa lengo za kuzituma katika mitandao ya kijamii ili
kumdhalilisha kinyume na sheria na kanuni ya adhabu.
Kosa la nne
ambalo ni wizi, ilidaiwa mshitakiwa alimnyanganya mtumishi huyo kiasi
cha pesa taslimu Tsh 50,000, power bank, chaji, airphone, simu mbili za
aina ya Son na Tecno vyote hivyo vikiwa na thamani ya Sh Mil 1,405,000.
Hata
hivyo mshitakiwa alikana makosa hayo, ambapo aliachiwa baada ya kupata
dhamana, huku hakimu wa mahakama hiyo akiahirisha kesi hadi tarehe
2/04/2015.
Hata hivyo mshitakiwa huyo wakati anatenda makosa hayo
alishirikiana na askari polisi kituo cha polisi Bariadi, ambaye
hakuweza kupatikana jina lake, huku taarifa zikisema kuwa askari huyo
bado anashugulikiwa na mamlaka zilizoko chini yake kijeshi.
Mshtakiwa
anadaiwa kutenda makosa hayo nyumbani kwake huko Kidinda na kwamba
chanzo kinasadikiwa ni wivu wa mapenzi ambao ulipelekea kumtuhumu
mtumishi huyo kuwa anatembea na mume wake.