Serikali ya Kenya imeutambua rasmi mwili wa mtu mmoja uliopatikana katika mbuga ya wanyama ya Tsavo, kuwa ni wa Meshack Yebei ambaye alikuwa shahidi katika kesi inayomkabili makamu wa rais wa Kenya William Ruto. kwenye Mahakama ya ICC.
Mkemia wa serikali ya Kenya ametangaza
kuwa mwili huo ambao ulikuwa umehifadhiwa kwenye chumba cha maiti tangu
mwezi December mwaka 2014 ni wa Meshack baada ya mwili huo kufanyiwa uchunguzi wa chembechembe za DNA.
Meshack Yebei
alitekwa mwishoni mwa mwezi December nyumbani kwake Eldoret alipokwenda
kumwona mkewe aliyekuwa anaumwa, familia yake ililalamika kuwa kutoweka
kwa Yebei kunatokana na kuhusishwa na kesi hiyo.
Yebei alitarajiwa kuwa shahidi wa Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto kwenye kesi yake ya mauaji inayoendelea Mahakama ya ICC, The Hague.
Marehemu alipewa nafasi ya kupata ulinzi
na makazi salama lakini akakataa, Serikali ya Kenya itafanya uchunguzi
kugundua kilichosababisha kifo chake.