Kutokana na Mvua zilizosababisha maafa Mkoani Shinyanga na kusababisha
watu 42 Kufariki na 91 kujeruhiwa Mkuu wa mkoa huo amewataka wananchi
waishio maeneo ya mabondeni kuhama ili kuepuka madhara kujitokeza
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Akitoa
Tahadhari hiyo kwa wakazi wa Mkoa huo Ally Nassoro Rufunga amesema kuwa
kwa mujibu wa mamlaka ya hali ya hewa walishatoa taarifa kuhusiana na
mvua hizo na serikali ilichukua hatua ya kuwaelemisha wananchi waishio
mabondeni kuhama na kuongeza kuwa kwa sasa wananchi wafate maagizo hayo
kwa kuwa mvua zitaendelea kunyesha.
Akitoa takwimu za Ujumla za Madhara yaliyojitokeza kutokana na mvua
hizo Rufunga amesema jumla ya kaya 82 zimeharibiwa na watu waliotharika
ni 574 na nyumba zilizoharibika kabisa ni 137, pamoja na Mashamba na
mifugo vimeharibika kabisa na jumla ya waliofoariki ni 42 na majeruhi ni
91.
Rufunga amesema mpaka sasa majeruhiwa wanaendelea vizuri na hali kwa
sasa juu ya matibabu na dawa serikali imeweza kulisimamia ingawa kwa
michango inaendelea ili kuweza kuwakimu walioathirika na maafa hayo.
Aidha amesema kwa sasa kambi ni moja ambayo wameiweka katika shule
ya msingi makwaka lakini jitihada za kutafuta maehma ili kuwahamishia
waathrika katika maeneo ya muinuko inaendelea.