SERIKALI IPO MBIONI KUIFUNGIA MITANDAO YA KIJAMII REDIO, NA TV ZINAZOFANYA MAMBO HAYA HAPA

Mamlaka  ya Mawasiliano Tanzania  (TCRA), imesema iko mbioni kuifungia mitandao ya kijamii, redio na televisheni inayokiuka maadili ya Mtanzania.

Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo, Innocent Mungy, alisema kuwa mitandao hiyo ni pamoja na  facebook, whatsapp na  instagram.

Alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu changamoto zinazoikabili mamlaka hiyo kutokana na kuwapo kwa watumiaji wengi wa mitandao hiyo katika kuelekea Siku ya Mawasiliano duniani inayofanyika Machi 15, kila mwaka.

Mungy alisema kuwa Mamlaka hiyo inafanya utafiti ili kubaini mitandao inayoongoza kwa kulalamikiwa na wateja ili hatua zichukuliwe.

Tangu TCRA iwezeshe kuwa na wingi wa simu na kuwezesha kuwepo kwa mitandao mingi ya kijamii changamoto zimeongezeka, maadili yameporomoka tofauti na miaka ya nyuma wakati kuna redio moja tu maadili yalizingazitiwa, kwa sasa utasikia lugha za matusi kwenye radio ikiwa ni pamoja na vipindi visivyofuata maadili na kanuni za habari, tuna mpango wakuifungia mitandao hiyo na vyombo vya habari visivyokidhi mahitaji,” alisema.

Alisema kuwa Mamlaka hiyo lengo lake ni kuwezesha Watanzania kwenda na wakati na kuelewa mambo mengi kwa wakati mmoja ikiwa ni pamoja na kupata habari ndani na nje ya nchi na kuongeza ajira kwa Watanzania kama ilivyo kwenye makampuni ya simu.

Aliwataka wamiliki wa mitandao kufuata maadili ikiwa ni pamoja na viongozi wa dini, wazazi, kuwafundisha wananchi na waumini wao kuwa na maadili ili kuondoa upotofu huo ambao unaweza kugeuza kizazi kisichofuata maadili na wengine kukosa ajira kutokana na kutumia mitandao vibaya.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo