RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete,
mapema leo amefanikisha uzinduzi wa Kituo cha Runinga cha Azam kilichopo
maeneo ya Tabata jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye uzinduzi
huo Rais Kikwete, alisema amefurahishwa sana na ubora wa studio hizo
kwani uwepo wake umeweza kututoa kimasomaso Watanzania wote kwa ujumla
kwani studio hizo zina hadhi namba moja kwa Afrika Mashariki na Kati.
Rais Kikwete akitoa hotuba fupi kwenye hafla hiyo.
Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam Media Group, Tido Muhando akiongea jambo kwenye uzinduzi huo.
Rais Kikwete akishuka ngazi baada ya kumaliza kuangalia moja ya studio iliyopo kwenye moja ya magari ya kurushia matangazo.