Hukumu
ya kifo kwa watuhumiwa wa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi
iliyotolewa na mahakama kuu imeibua hamasa na mitazamo tofauti kwa
wananchi ambao pamoja na kupongeza hatua hiyo wamesema wanachosubiri
sasa ni kuona ngazi zinazohusika zikitekeleza hukumu hiyo.
Wananchi hao wamesema ili adhabu hiyo iweze kuwa na tija na kuwa
fundisho kwa wengine ni vyema utelezaji wa hukumu iliyotolewa ufanyika
haraka na jamii ione huku wengine wakitaka kesi zinazohusiana na
mauaji ya albino zitenganishwe na kesi zingine ili zisichukue muda
mrefu.
Katika hatua Bi.Ester Mahawe ambaye ni mkurugenzi wa shule ya
Intel School ya mkoani arusha amejitolea kuwasomesha watoto wawili
wenye ulemavu wa ngozi ambao mdogo wao aliuawa hivi karibuni huko
geita.
Akitangaza azima yake hiyo Bi.Ester amesema baada ya kutafakari
kwa muda amebaini kuwa anachoweza kusaidia ni kuwalea na kuwasomesha
watoto hao,Shija Bahati (11) na Aseri Bahati (2) kuanzia elimu ya awali
hadi darasa saba.