NYUMBA YAUNGUA KWA MOTO WA AJABU,YADAIWA NI MAJINI,WENYE NYUMBA WATANDIKWA MAKOFI WAKIWA USINGIZINI

Wakazi wa Kijiji cha Ivaini Kenya wamejawa na hofu baada ya nyumba ya mzee mmoja kuteketezwa kwa moto na viumbe visivyoonekana ambapo ishu hiyo inahusishwa na imani za kishirikina.
Mzee huyo Mukai Kimanzi amesema nyumba yake iliteketezwa na majini yanayoiandama familia yake na yamekuwa yakimkosesha usingizi, yanamtia hofu.. kuna wakati yanawapiga makofi  wakiwa wamelala.
“Waliniambia waliona moto tu unachoma kila kitu kwa kweli nyumba.. moja imechomeka na nyingine bado zinachomeka, kulingana vile mimi naona, mimi naona ni mapepo tu” Mzee Mukai Kimanzi.
Majirani wa eneo hilo wamesema nyumba hiyo imeteketezwa na mapepo mabaya na kudai kuwa huwa hali inakuwa tofauti inapotimia saa moja usiku, yeyote atakaesogea eneo hilo anarushiwa mawe na majini hayo.
Mzee huyo amelazimika kuondoka nyumbani kwake na kuishi kwa ndugu yake ambae nae anataka kumfukuza mzee huyo kutokana na hofu kwamba atavamiwa na majini hayo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo