Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe amesema atafanya kazi kukijenga Chama cha ACT kama alivyofanya kazi akiwa CHADEMA.
Zitto ametaja sababu tano zilizofanya avutiwe na Chama hicho kuwa ni pamoja na misingi ya Chama hicho kujali maslahi ya Taifa, itikadi za Chama hicho kukubaliana na ujamaa, pia kukubaliana na imani ya ACT inayosimamia umoja.
Kuhusiana na ishu ya usaliti wake kwa CHADEMA Zitto Kabwe amesema; “Naombeni mjaribu kufumba macho yenu mjiulize ni Mbunge gani katika Bunge hili ametoa hoja ambazo zilikitikisa CCM. Mara mbili nimetoa hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.. Mara mbili nimeng’oa Mawaziri wa CCM, wanane 2011.. Suala la ESCROW nimeng’oa Mawaziri watatu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.. swali la usaliti walitakiwa kuulizwa hao ambao wako Bungeni hawafanyi kazi kuiwajibisha Serikali”—Zitto Kabwe.
Wakati wa Mkutano huo wa Zitto chama cha ACT kilivuna wanachama wapya zaidi ya kumi wakiwamo waliokuwa viongozi wa TLP, CHADEMA na CCM.
DIRA
Utafiti uliofanywa na Shirika la Utangazaji la BBC unaonesha kuwa kati ya wanawake watatu Afrika mmoja kati yao anatumia mkorogo, wanawake hao wanatumia vipodozi vikali vyenye Mercury mara 60 zaidi ya kiwango ambacho kimekatazwa.
Katika tafiti za Shirika la Afya WHO 77% ya wanawake duniani wanatumia vipodozi hivyo vya kung’arisha ngozi, huku ikielezwa kuwa katika kila wagonjwa 10 wa saratani ya ngozi, wanne kati yao hupata tatizo hilo kutokana na matumizi ya mkorogo.
“Baadhi ya wanawake wamekuwa wakipata madhara kutokana na kutumia vipodozi vyenye sumu kwa muda mrefu hivyo sumu wanayoitengeza kwa muda mrefu ndiyo huleta madhara makubwa kiafya..” aliongea Gaudensia Simwaza, Afisa Uhusiano wa TFDA.