Idadi
hii inawakilisha maisha halisi na kuonesha kwamba kama jitihada za
makusudi hazitachukuliwa wasichana wataendelea kukosa haki zao za msingi
na kuzidi kuwa wategemezi.
Hayo
yalisema na mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akifungua mkutano wa
kimataifa wa utafiti katika ukunga ulioandaliwa na LUGINA Afrika
Midwives Research Network (LAMRN) uliofanyika katika Hoteli ya Kunduchi
jijini Dar es Salaam.
Mama
Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA)
alisema vifo vya akinamama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya
miaka mitano ni tatizo katika nchi zote zilizopo Kusini mwa Bara la
Afrika hata hivyo jitihada mbalimbali zinafanyika ili kuhakikisha tatizo
hilo linapungua au kumalizika kabisa.
“Naamini
utafiti uliofanywa na LAMRN kwa kipindi cha miaka miwili, utasaidia
kuongeza utendaji kazi wa wakunga na kupunguza vifo vya akinamama
wajawazito na watoto katika bara letu la Afrika,” alisema.
Kuhusu
mimba za utotoni Mwenyekiti huyo wa WAMA alisema tafiti zilizofanyika
zinaonesha wasichana wanaanza kufanya mapenzi mapema zaidi wakiwa na
umri mdogo ukilinganisha na wavulana jambo linalopelekea kupata mimba za
utotoni na hivyo kukosa elimu kwa kukatisha masomo yao.
Mama Kikwete alisema: “Takwimu
za Ulimwengu zinaonesha zaidi ya wasichana milioni 58 wameolewa kabla
ya kufikisha umri wa miaka 18 kati ya hao milioni 15 wana umri wa miaka
10 hadi 14.
"Nchini
Tanzania asilimia 13 ya wasichana wanaanza kufanya mapenzi wakiwa na
umri wa miaka 15 na kwa upande wa wavulana kwa umri huo huo ni asilimia
saba".
