Vurugugu hizo zimedumu kwa muda ambapo wananchi walipanga mawe
barabarani na kuzuia magari yanayotumia barabara hiyo wakilalamikia
kuchoshwa na matukio ya ajali za mara kwa mara katika eneo hilo
wakiitaka serikali kuweka matuta.
Kufuatia vurugu hizo za wananchi, serikali ya kijiji na mkuu wa
polisi wilaya Zuberi Chembela na wamelazimika kutuliza wananchi hao
waliokuwa wakizungumza kwa jazba na kuwaahidi jeshi la polisi litaweka
ulinzi katika eneo hilo kuzuia matukio ya ajali.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Lenard Paul amesema chanzo cha
tukio ni gari ndogo kugonga wapanda pikipiki Godwini Mbena na alikua
amempakiza mkewe Judith Mbega mwalimu wa shule ya msingi Mkambarani
ambaye alifariki dunia na mumewe amejeruhiwa na kulazwa katika hospitali
ya mkoa wa Morogoro ambapo amesema jeshi la polisi litawachukulia
hatua wananchi waliohusika kufanya vurugu za kufunga barabara.